CHAGUA TAREHE YA KULIPA KODI:


JAZA KIASI CHA KODI UTAKACHOLIPA:


JAZA NAMBA YAKO YA SIMU:






YOUR ACCOUNT HAS BEEN BANNED.

CHAKIWA NI NINI?
Chakiwa ni chama kidogo cha wapangaji/walipa kodi, ambacho kimeanzishwa kwa dhumuni la kuwasaidia wanachama wake kuweza kulipa kodi zao kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kufungiwa nyumba/chumba, ofisi, au kudhalilishwa endapo watakuwa hawajaweza kupata hela ya kutosha kulipa kodi zao kwa wakati.

Chakiwa itakuwa inakuongezea kiasi cha hela kilichopungua kwenge hela yako unayotakiwa kulipa kodi, tarehe yako ya kulipa kodi inapofika.

Mfano: Tarehe yako ya kulipa kodi imefika na unatakiwa kulipa kodi ya shilingi 600,000/= na wewe kiasi ulichonacho ni 400,000/=. Kwahiyo Chakiwa itakuongezea 200,000/= iliyopungua ili kumalizia kulipa kiasi chote.

Ili kuwa mwanachama wa Chakiwa, unatakiwa kulipa ada ya uanachama mara moja tu yaani pale unapotuma taarifa za tarehe yako ya kulipa kodi. Kiasi cha ada mwanachama anachotakiwa kulipa ni kuanzia 5,000/= au zaidi kwa kutegemea jumla ya kiasi cha kodi anayotakiwa kulipa.

Tarehe yako ya kulipa kodi uliyoijaza ikifika unatakiwa kuingia kwenye akaunti yako ya Chakiwa, kwa kutumia namba yako ya simu uliyoijaza wakati unatuma taarifa zako za tarehe ya kulipa kodi. Ukishaingia unabonyeza sehemu imeandikwa "Omba Ruzuku" ili kuomba kiasi cha fedha utakachokuwa umepungukiwa.

Na unaweza kuweka tarehe za malipo ya kodi zaidi ya moja, kama unasehemu tofauti tofauti za kulipa kodi.

Ruzuku ya kodi husika unaweza kuiomba ndani ya siku mbili kutoka siku yako ya kulipa kodi ilipofika. Kama siku mbili zimepita na hujaomba ruzuku yako ya kodi kwa tiketi husika, hutaweza kuomba tena ruzuku kwa tiketi hiyo kwa maana system inatambuwa ulishaweza kulipa kodi yako yote mwenyewe.